WAKATI wananchi, ndugu, jamaa na marafiki
wakiendelea kuusubiri mwili wa aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko
ya katiba marehemu Dk. Sengodo Mvungi kutoka Afrika Kusini alikopelekwa
kwa matibabu, viongozi mbali mbali wameendelea kuzungumzia utashi na
ufanyaji kazi wake enzi za uhai wake.
Akizungumza na 100.5 nyumbani kwa Marehemu Kibamba Jijini Dar es
Salaam, Mwanadiplomasia ambaye pia ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya
katiba Dkt.Salim Ahmed Salim, amesema wataikosa michango mingi ambayo
alikuwa akiitoa marehemu katika mikutano yao.
Mwili wa marehemu Dr. Mvungi utawasili leo nchini na siku ya Jumamosi
kutakuwa na ibada maalum ya marehemu kwenye Kanisa la Mt. Joseph na
baadaye mwili wake utaagwa kwenye viwanja vya Karimjee kabla ya
Jumapili kusafirishwa kwenda Kisangara Wilayani Mwanga Mkoa wa
Kilimanjaro kwa mazishi
Mwanzoni mwa mwezi huu Dk Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu
wanaosadikika kuwa ni majambazi nyumbani kwake na alhamis iliyopita
alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi, hadi
mauti yalipomfika
Wakati huo huo, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein hii leo amemtumia salamu za
rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba kufuatia kifo cha Dk. Sengondo Mvungi.
Katika salamu zake hizo, Dk. Shein amemuelezea marehemu Dk. Mvungi
kuwa ni mzalendo mwenye upendo mkubwa kwa nchi yake, mtaalamu wa sheria
na Vilevile mwanasiasa shupavu na makini,hivyo anamchango mkubwa sana
katika taita lake.
No comments:
Post a Comment