Dar es Salaam.Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,imekamata vielelezo vya mtu anayedaiwa kuiba Kompyuta Mpakato (laptop) ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi.
Kamishna wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova
alitaja vielelezo hivyo kuwa ni pamoja na picha ya mtuhumiwa anayedaiwa
kuiba kompyuta hiyo (jina linahifadhiwa).
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi wa kipolisi
unaonyesha kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye bado hajakamatwa anadaiwa
kujihusisha na masuala mbalimbali ya uhalifu jijini Dar es Salaam.
Alisema kompyuta hiyo inadaiwa ilikuwa na taarifa muhimu za kikazi za Dk Mvungi.
“Vielelezo vilikamatwa wakati polisi wakiwa kwenye msako wa kuwatafuta wahusika wa tukio la mauaji ya Dk Mvungi” alisema.
Kamanda Kova aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya mtuhumiwa huyo anayedaiwa bado anaimiliki kompyuta ya Dk Mvungi.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema,
polisi inamshikilia mtu aliyedaiwa kujifanya askari,aliyeachishwa kazi
mwaka 2003 katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Askari huyo anadaiwa kukamatwa katika eneo la
Mivinjeni akiwa na mtuhumiwa mwingine mkazi wa Kinondoni B, wakiwa
katika harakati za kupora gari aina ya Kenta lililokuwa limebeba sigara
zenye thamani ya Sh200 milioni.
Kova alisema, uchunguzi umebainika watuhumiwa hao
pia ni washiriki kwenye matukio ya wizi wa fedha kwenye Benki za Habib
na I&M za Dar es Salaam.chanzo mwananchi
No comments:
Post a Comment