Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya Mkoani
Geita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyo
itumike kuwasaidia watoto yatima.
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013,
baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua
mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa
Kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale,Mkoa wa
Geita.
Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.
Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: “Sasa nifanye
nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka
na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”
Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza
uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya
maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.
Hatahivyo, Rais Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada
za kuboresha teknolojia inayotumika. “Mmefanya vizuri sana na mgodi huu
ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha
maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia
inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na
hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye
anaonekana kama mfalme.”
Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba
unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa
nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa
kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.
Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi
chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemo
wanawake 10.
Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za
jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa
yashule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa
waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa
mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.
Ziara hiyo ya siku tano inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na
mbali ya kuzindua mgodi huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya
maendeleo ya Wilaya ya Nyang’hwale na kuhutubia mkutano wa hadhara
katika mji mdogo wa Kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya
wananchi.
Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!
Imetolewana:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
No comments:
Post a Comment