Taasisi
za Fedha nchini zimepoteza kiasi cha Sh34.4 bilioni kuanzia kipindi cha
Oktoba mwaka jana hadi Oktoba mwaka huu kutokana na wizi wa fedha katika
taasisi hizo,ripoti mpya imebainisha.
Utafiti huo
uliofanyika katika nchi za Kenya,Tanzania na Uganda umebainisha
kuwa,Taasisi za Fedha za Afrika Mashariki zimepoteza zaidi ya Sh471
bilioni sawa na (USD 30 milioni) kwa mwaka.
Hata
hivyo benki hizo ziliweka wazi upotevu wa Sh126.9 bilioni tu ambao ni
robo ya upotevu huo wa zaidi ya Sh471 bilioni kwa kile kinachodaiwa
kuhofia kupoteza wateja.
"Taasisi
za fedha zinapoteza fedha nyingi kutokana na teknolojia na watendaji wa
ngazi za juu kuhusika kwa kiwango kikubwa lakini hazitaki kukiri kwa
sababu ya kuhofia kukosa wateja," alisema Robert Nyamu, Mkurugenzi wa
Delloite, Afrika Mashariki.
Msemaji
wa Benki Kuu ya Tanzania,Loy Nabeta hakuwa tayari kuzungumzia upotevu
huo na kusema kuwa ni suala linalohitaji majadiliano ya kina na utendaji
wa ngazi za juu.
Wimbi la
wizi wa fedha katika benki lilianza kupata umaarufu mwaka 2010 na Oktoba
2012 hadi Februari 2013, inakadiriwa kuwa jumla ya Sh700 milioni
zimeibwa katika benki mbalimbali kwa nyakati tofauti.
Ripoti
hiyo ya Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2013 iliyotolewa na Kampuni ya
Uchunguzi wa Huduma ya Delloite imebaini kuwa watendaji wa ngazi za juu
wanahusika zaidi na uhalifu huo ukilinganisha na watendaji wa ngazi za
chini.
"Wanapofanya
uhalifu hujua namna ya kuuficha na kuujadili na wasimamizi wa ndani
bila kubainika.Wanajua mbinu na mifumo yote ya kifedha na wanatumia
fursa hiyo kuiba," alisema Nyamu.
Watendaji
waliotajwa kuhusika zaidi na wizi huo wa fedha ni wale wa ngazi za juu
wakiwamo wakurugenzi watendaji, ofisa operesheni, wakurugenzi wa fedha,
vitengo vya teknolojia na wakuu wa vitengo wanatumia nafasi zao kufanya
uhalifu wa fedha ukilinganisha na wafanyakazi wa kati na ngazi za chini.
Wizi
unaofanyika zaidi katika nchi za Afrika Mashariki unatajwa kuwa ni wa
fedha halali ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya uhalifu wa aina zote wa
kifedha.
Hata
hivyo Nyamu alisema watendaji wa ngazi za chini wanaweza kufanya uhalifu
wa kiasi kikubwa cha fedha iwapo wanajua namna ya kufanya hivyo.
Mtaalamu
wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM), Dk Eliamani
Sedoyeka alisema ni kweli kuwa watu wa ngazi za juu wanatumia nafasi zao
kufanya uhalifu wa kifedha kwa sababu wanaelewa kwa undani mfumo
unavyofanya kazi na kutolea mfano i wizi wa Benki ya Stanbic .chanzo matukio na michapo blog
No comments:
Post a Comment