Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 21, 2013

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU SHUGHULI PEMBEZONI MWA RELI



 Serikali imepiga marufuku wananchi kufanya shughuli zote  za kibinadamu pembezoni mwa hifadhi zaareli ikiwemo kujenga nyumba, kulima au kufanya biashara na kuagiza watu wote ambao wanajihusisha na shughuli hizo kuondoka haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili kuepusha uharibifu wa reli na madaraja unaochangiwa watu hao na kulisababishia taifa hasara kumbwa.

 Kauli hiyo ya saerikali inatolewa na naibu waziri wa uchukuzi Mhe Charles Tizeba wakati akifanya ziara ya kutembelea madaraja ya treni yaliyopo  wilayani Bahi mkoani Dodoma ambapo amesema shuguliza kubinadamu zinazofanyika pembezoni mwa hifadhi za reli zikiwemo kilimo na kupitisha mifungo juu ya reli zinaweza kusababisha reli na madaraja kusombwa na maji kipindi cha mvua.

No comments:

Post a Comment