Wekundu
wa Msimbazi Simba Sc, leo hii wamefufuka baada ya ushindi wa mabao 4-2
dhidi ya Ashanti United katika mchezo wao wa kufunga pazia la mzunguko
wa kwanza ligi kuu soka Tanzania bara.Mabao ya Simba yamefungwa na Ramadhan Singano `Messi` , Betram Mwombeki aliyefunga mawili na Amissi Tambwe.Ashanti wao wamejipatia mabao yao kupitia kwa Hussein Swedi na Mkongwe Said Maulid `SMG`.Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, hadi mapumziko
tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1.
Timu
hizo zilishambuliana kwa zam ambapo Ashanti walipiga pasi nzuri na
fupifupi wakati Simba wao walikuwa wanapiga mipira mirefu.
Licha
ya ushindi huo, Simba sc wanabakia katika nafasi ya nne wakiwa na
pointi zao 24, huku Yanga wakiwa nafasi ya tatu na pointi 25, Mbeya City
na Azam fc wapo juu kwa pointi 26 na timu zote kesho zinacheza mechi
za kukamilisha ratiba ya mzunguko wa kwanza.
Mchezo
mwingine umepigwa katika dimba la Azam Complex ambapo JKT Ruvu walikuwa
wanakabiliana na Coastal Union na maafande hao kuibuka na ushindi wa
bao 1-0.
Ruvu
Shooting walikuwa na kibarua mbele ya Mtibwa Sugar katika uwanja wao wa
Mabatini na kushuhudia timu hizo zikichoshana kwa sare ya bao 2-2.
Kagera Sugar wamekamilisha ligi kuu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo Jkt katika dimba la Kaitaba.
Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara utamalizika kesho kwa mechi Tatu kupigwa viwanja vitatu tofauti.
Yanga
watakuwa uwanja wa Taifa kuwakabili JKT Oljoro, Azam fc watakuwa
wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wao wa Azam Complex, nao Maafande wa
Rhino Rangers watakuwa nyumbani Ali Hassan Mwinyi kuwakabili Tanzania
Prisons.
No comments:
Post a Comment