NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM
MBUNGE wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), leo anatarajia kuanza kukusanya
saini za wabunge kwa ajili ya kumuondolea dhamana waziri
anayeshughulikia habari, kutumia kifungu cha 25 cha sheria ya mwaka 1976
ya kuyafungia magazeti.
Mbilinyi
maarufu kwa jina la Sugu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo,
alisema baada ya kukusanya saini hizo atawasilisha bungeni hati ya
haraka ya muswada binafsi wa sheria ya marekebisho ya sheria ya magazeti
ya 1976, kwa lengo la kurekebisha kifungu cha 25 kinachotumiwa vibaya
na waziri kuvifungia vyombo vya habari kutochapisha habari.
Akizungumza
na RAI Jumatatu jana alisema kutimiza masharti ya kanuni ya uwasilishaji
wa hati binafsi, amewaomba wabunge kutia saini kwa lengo la kumuunga
mkono ili vyombo vya habari viweze kufanya kazi yake vizuri.
Alisema
ameamua kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu zote za muswada za sheria
utaolazimika kuchapwa kwanza katika gazeti la Serikali.
"Kwa
vyovyote vile Serikali itatumia kisingizio cha kesi iliyofunguliwa na
Hali Halisi Publishers ya mwaka 2009, ambayo ilifunguliwa baada ya
Gazeti la Mwanahalisi kufungiwa.
"Lakini
hadi leo kesi haijasikilizwa ambapo Serikali inafanya makusudi
kuchelewesha kusikilizwa kwa kesi hiyo ndani ikiwa sasa ni miaka minne
na sheria hiyo imeendelea kuyafungia magazeti mengine.
"Hivyo
basi kukwepa kikwazo hicho, nitawasilisha muswada wa dharura wa kufanya
marekebisho, sio kufuta bali kumwondolea waziri mwenye dhamana mamlaka
ya kufungia, kusitisha kuchapisha gazeti lolote au magazeti yoyote.
"Serikali
haitaweza kutumia kisingizio cha kesi iliyo mahakamani kufanya
marekebisho ya sheria hiyo, kwa sababu pamoja na kesi kuwapo mahakamani,
tayari imeshasoma kwa mara ya kwanza bungeni Muswada wa Marekebisho ya
Sheria mbalimbali namba tatu wa 2013 ambao katika vifungu vya 40 na 41
inakusudia kufanyia marekebisho vifungu vya 36(1) na 37 (1) (b).
"Kwa ajili ya kuongeza faini kwa magazeti kutoka Sh 150,000 hadi Sh milioni tano kwa makosa ya kashfa," alisema.
Hivi
karibuni, Serikali imeyafungia magazeti mawili likiwamo la MWANANCHI kwa
siku 14 na MTANZANIA siku 90 ambalo hadi sasa linaendelea kutumikia
kifungo hicho.
Serikali
ilitumia sheria hiyo ambayo inampa dhamana waziri husika kuchukua hatua
dhidi ya gazeti husika lililochapisha habari ya kashfa.
No comments:
Post a Comment