Wafanya biashara wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamekusanyika wakijadili jambo.
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.Wafanya biashara hao wamegoma kufungua maduka tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa jambo ambalo Mkuu wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8 kwa ajili ya kwenda kuonana nao.Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado wafanyabiashara hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndipo Jeshi la Polisi walipoingilia kati .
Jeshi la Polisi wakiwa barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na wafanyabiashara hao muda huu.
Waduka yakiwa yamefungwa katikati ya Mji wa Morogoro

No comments:
Post a Comment