skip to main |
skip to sidebar
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA::MTOTO AKATWA VIBAYA USONI NA KITU CHENYE NCHA KALI MKOANI SONGEA.
Wakati
Dunia ikipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto hapa nchini Bado vitendo hivyo vimeonekana vikiendeleea ambapo
MTOTO Mmoja BENSON TOLE mwenye umri wa miaka Mitano mkazi wa Ruhuwiko
mjini Songea mkoani Ruvuma, amenusurika kifo baada ya kukatwakatwa kwa
kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na Mzee mmoja LONGINUS HAULE
mwenye miaka 51 akimtuhumu mtoto huyo kumuibia matunda aina ya Mapera shambani kwake.
EMMANUEL MSIGWA kutoka mjini Songea
Mtoto BENSON TOLE kwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini
Songea katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU), Madaktari wanaendelea
kunusuru uhai wa mtoto huyu baada ya kupata mashambulio makali ya
kucharangwacharangwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na
mtuhumiwa mmoja LONGINUS HAULE mkazi wa Polisi Lizaboni mjini Songea.
Mzee HAULE anatuhumiwa baada ya kumfanyia unyama wa kutosha mtoto huyo
na kisha kupoteza fahamu akimtuhumu kumuibia matunda aina ya mapera
shambani kwake alimtupia kwenye nyumba moja ambayo haijaisha ujenzi wake
akidhani tayari ameshamuua.
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa
mjini Songea, JOSEPH MTEWELE amesema kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya
uangalizi maalumu na kwamba madaktari wanaendelea na jitihada za
kunusuru uhai wake kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata sehemu za
kichwani.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limetihibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba linaendelea kuchukua hatua zaidi za kumfikisha
Mzee LONGINUS HAULE kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment