Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mfanyabishara wa magari kutoka jijini Mwanza,amemuua mwanamke mmoja na kujeruhi vibaya watu watatu kwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao katika eneo la ilala jijini Dar es Salaam na kisha kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi.
Waandishi wa ITV walifika katika eneo la tukio ambalo lipo karibu kabisa
na hoteli ya MM eneo la Ilala jijini Dar es Salaam na kushuhudia watu
mbalimbali wakiwa wamezunguka eneo hilo huku gari aina ya Toyota Hilux
Surf yenye namba za usajili T.537 iliyokuwa ikitumiwa na familia hiyo
ikiwa imeharibiwa vibaya kwa kupigwa risasi huku damu zikienea ndani ya
gari na maeneo mbalimbali ambapo baadhi ya mashuhuda wamesema.
Mkuu wa upepelezi kanda maalum ya Dar es Salaam kamishna msaidizi wa
polisi Ahmed Msangi aliyewahi kufika katika eneo la tukio akiongozana na
maafisa wengine wa jeshi la polisi, amesema aliyefanya mauji na
kujeruhi watu watatu anaitwa Gabriel Munisi ambaye amedaiwa kuwa ni
mfanyabishara wa magari kutoka jijini Mwanza, huku aliyeuawa kwa kupigwa
risasi kichwani amejulikana kwa jina moja la Alfa,huku majeruhi wengine
kama Francis Samwel ambaye alikuwa dereva wa gari iliyokutwa hapo
amepigwa risasi kifuani,mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Hellen
Elieza amepigwa risasi ya begani kulia kwa nyuma na Bi Christina Nando
Newa anayedaiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyabishara
huyo aliyejiuwa alipigwa risasi ya paja.
Ndugu wa familia hiyo bwana Mloy Newa,amedai ndugu zake waliondoka na
gari hilo hapo nyumbani kumsindikiza dada yao Bi Christina Nando Newa
ambaye anadaiwa alikuwa akisafiri kwenda Saipraz na baadhi yao walikuwa
wakienda makazini huku mkuu wa kitengo cha dharura kutoka hospitali ya
amana dakta Christopha Mzava akithibitisha kupokea majeruhi na miili ya
marehemu katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment