Tanga.Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametangaza vita rasmi na
wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu
mkoani Tanga na maofisa wa vyombo vya Serikali waliopo kwenye mtandao
huo.
Dk
Mwakyembe aliwataka watambue kuwa, kiama chao kimefika kwa sababu
tayari Serikali inayo majina ya wafanyabiashara na baadhi ya maofisa wa
polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA)
wanaotumika kufanikisha upitishaji magendo.
Dk
Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi na kufanya ziara ya ghafla
kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani hapa, alitangaza vita hiyo
alipozungumza na maofisa wa TRA, polisi, TPA na wafanyabiashara.
Alisema
baada ya Serikali kudhibiti Bandari ya Dar es Salaam, wafanyabiashara
magwiji wa upitishaji bidhaa za magendo wamehamishia nguvu zao Tanga.
“Natangaza
rasmi vita dhidi ya walio katika mtandao huo, watambue hatuwezi
kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari bubu na mpaka wa Horohoro kuwa gulio
la walanguzi, wapitishaji dawa za kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
No comments:
Post a Comment