Dar es Salaam. Bodi ya Ligi (TPL) imefunga viwanja saba vilivyokuwa vikitumika katika mzunguko wa kwanza Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kutokana na uchakavu na havifai kutumika kwa mashindano.
Hatua hiyo imefikiwa na bodi hiyo Jumapili
iliyopita baada ya kukutana kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake
ili kupitia ripoti mbalimbali zilizokuwa zikihusiana na mzunguko wa
kwanza wa ligi hizo uliofika tamati hivi karibuni.
Viwanja vilivyofungiwa ni Ali Hassan Mwinyi wa
Tabora, Mkwakwani (Tanga), Kaitaba (Bukoba), Jamhuri (Morogoro), Sokoine
(Mbeya), Majimaji (Songea) na Sheikh Amri Abeid (Arusha).
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Boniface Wambura alisema kuwa viwanja vya Ali Hassan Mwinyi na
Mkwakwani vimefungiwa kutokana na vyumba vya kubadilisha nguo kuwa ni
vibovu.
Alisema vyumba vya Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi pia
vimekuwa vikitumika kama shule ya chekechea wakati Uwanja wa Kaitaba
majukwaa yake ni mabaovu na yatishia usalama wa watu wanaofika uwanjani
hapo.
“Hata hivyo viwanja vya Jamhuri Morogoro, Sokoine, Majimaji na Sheikh Amri Abeid ubovu wake ni katika sehemu ya kuchezea.
“Kutokana na hali hiyo kamati imeagiza vifanyiwe
ukarabati, hivyo timu husika ambazo zinavitumia kwa ajili ya mechi zake
inabidi ziwasiliane na wamiliki wa viwanja hivyo kwa lengo la kufanyiwa
ukarabati mapema iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa
ligi hizo.
“Endapo mpaka kufikia muda huo kama itakuwa bado
havijafanyiwa ukarabati huo basi timu hizo zitalazimika kutafuta viwanja
vingine ambavyo vitakuwa vinakidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa
ajili ya michuano hiyo,” alisema Wambura.
Katika hatua nyingine kamati hiyo imezitoza faini
baadhi ya timu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza ikiwa ni pamoja na baadhi
ya wachezaji na viongizi wako kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu
kwenye muzunguko huo wa kwanza wa ligi hizo.
Timu ya Mbeya City imelimwa faini ya Sh 1.5
milioni kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu waliyofanya viongozi na
mashabiki wa timu hiyo.
Makosa hayo ni pamoja kutoingiza uwanjani kikosi
chake cha vijana kucheza mechi ya utangulizi kabla ya mchezo wake wa
LigiuKuu dhidi ya Coastal Union pia mashabiki wake kufanya vurugu wakati
wa mechi yake dhidi ya Yanga na Prisons.
Hata hivyo mbali ya faini hiyo pia wametakiwa
kulipa gharama za uharibifu uliotokana na fujo hizo ikiwa ni pamoja na
kuvunja vioo vya basi la Yanga, gharama hizo zitalipwa baada ya
kuthibitishwa na Kamati hiyo ya ligi.Timu nyingine zilizokumbana na
rungu la kamati hiyo ni Cocastal Union ambayo ililimwa faini ya Sh
500,000 baada ya wachezaji wake kufanya fujo katika mechi yao dhidi ya
Azam.chanzo mwanainchi
No comments:
Post a Comment