MOSHI - Mwanamke ambaye ambaye hajafahamika mara moja amefariki
dunia jioni Ya Jana katika mtaa wa Posta mjini Moshi kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea
baada ya kuacha njia na kumkuta mwanamke huyo.
Tukio hilo limetokea majira ya
saa 12: 45 za jioni.
Mashuhuda waliokuwepo katika
tukio hilo wamesema mwanamke huyo alikuwa ametoka katika shughuli za kibiashara
katika soko lililopo mjini hapo.
Duru za habari zimeendelea
kujuza kwamba mwanamke huyo ni Mnyakyusa aliyeolewa na Mchaga wote wakazi wa
KCMC Mjini hapa.
JAIZMELALEO
imekuwepo katika tukio hilo na kushuhudia gari aina ya Fuso lililosajiliwa kwa
namba T 209 AHA likiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika mara
moja.
Mashuhuda wanasema chanzo cha
ajali hiyo ni mwendokasi uliosababishwa na dereva wa Fuso aliyekuwa amelewa.
Wameongeza kuwa watu wawili
wamejeruhiwa kufuatia tukio hilo, ambao ni dereva wa bodaboda na rafiki yake
waliokuwa wamepaki pembezoni mwa mtaa huo wakisubiri wateja.
Dereva wa Fuso hilo lililokuwa na maandishi yanayosomeka "AINULIWE BWANA" anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Jeshi la Polisi limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali ya KCMC na taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo zitatolewa mpaka
pale upelelezi utakapokamilika.
CREDIT : JAIZMELALEO
No comments:
Post a Comment