Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli.
DAR ES SALAAM. WABUNGE watatu na madiwani wawili wa Kanda ya Ziwa,
wameshtakiwa mbele ya Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma kwa tuhuma
mbalimbali zikiwemo za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma.
Viongozi
hao pamoja na wanasheria watatu, akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Sengerema Liveti Msangi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wanasomewa
tuhuma zao hizo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Balozi, Jaji
Mstaafu Hamis Msumi na wajumbe wawili wa baraza hilo, Hilda Gondwe na
Celina Wambura.
Akizungumza
na waandishi wa habari Nov 15 mwaka huu, Kaimu Kamishna wa Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tixon Nzunda alisema baraza hilo
linaendelea kusikiliza kesi hizo mkoani Tabora, ambapo wananchi
wanaruhusiwa kusikiliza kesi hizo huku Sekretarieti hiyo ndiyo
mlalamikaji.
“Kama nilivyosema ni baraza la wazi, ni viongozi mbalimbali
walioshtakiwa huko, lakini kwa kuwa mimi simo miongoni mwa wanaoendesha
kesi hizo sipo tayari kuwatajia,” alisema Nzunda.
Hata hivyo,
habari za uhakika kutoka katika vyanzo vyetu vya habari, wabunge hao
wametajwa kuwa ni Lameck Airo (Rorya), Salvatory Machemli (Ukerewe) na
Suleiman Suleiman (Kishapu).
Madiwani
wanaoshtakiwa kwenye baraza hilo ni Mathias Bisoma (Kata ya Kanazi,
Kagera), Meya wa Jiji la Mwanza Henry Matata ambaye ni Diwani wa Kata ya
Kitangiri.
Viogozi
wengine walioshtakiwa na Sekretarieti ya Maadili katika Baraza hilo ni
Mwandishi Mkuu wa Sheria, Casmir Sumba Kyuki na Mkurugenzi Msaidizi
Uandishi wa Sheria, Sarah Kinyamfura Barahomoka.
Miongoni
mwa mashtaka yanayowakabili viongozi hao ni pamoja na matumizi mabaya ya
madaraka, huku wengine wakidaiwa kushindwa kuwasilisha matamko ya
rasilimali zao.
Awali,
Nzunda alifafanua kuwa kesi hizo zitasikilizwa kwa wiki mbili, ambapo
mashahidi ni wananchi. Baraza hilo ni taasisi huru inafanya kazi zake
kwa mara ya kwanza baada ya kuchanguliwa na kuapishwa na Rais Jakaya
Kikwete, Julai mwaka huu. MWANANCHI


No comments:
Post a Comment