Na Flora Martin Mwano
Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Joseph Kabila ameteua Tume maalumu
ya kitaifa kwa ajili ya usimamizi na utekelezaji wa maazimio
yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyofanyika hivi karibuni.
Rais Kabila pia amesaini sheria ya uundwaji wa Tume hiyo
itakayoshughulikia masuala kadhaa yanayohitaji utekelezwaji wa
dhati.Katika uteuzi huo wametajwa pia Maspika wa Bunge la Taifa na lile
la Seneti watakaoisimamia Tume hiyo.
Aidha,
Rais Kabila amewajumuisha wakuu wa kamati za majadiliano ya kitaifa na
watendaji wa ngazi ya chini katika Tume hiyo kwa vile wameziongoza
kamati zao katika muda wote wa majadiliano ya kitaifa.
Mwezi
uliopita, Rais kabila alihutubia taifa na kuhitimisha mazungumzo ya
kitaifa na kutoa ahadi kadhaa kwa ajili ya mshikamano nchini humo
ikiwemo uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa itakaojumuisha wadau
kutoka pande zote hasa vyama vya upinzani.
Kwa
upande mwingine, baadhi ya vyama vya upinzani vyenye msimamo mkali
vimetupilia mbali pendekezo hilo la Rais kabila na kubainisha kuwa
kilicho cha muhimu ni kuweka misingi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 kwa
vile Rais huyo anaelekea mwishoni mwa muhula wake wa pili.


No comments:
Post a Comment