Wanaume wanne wamefikishwa
mahakamani nchini Kenya baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi
lililofanyika dhidi ya jengo la Westgate nchini Kenya mwezi Septemba.
Wanne hao wote walikanusha mashitaka hayo
ikiwemo kosa la kuingia nchini bila vibali halali pamoja na kumiliki
stakabadhi bandia za kujitambulisha.
Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.
Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate wakati wa shambulizi hilo.
Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan.
Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment