Kamanda Suleiman Kova akiongea na wanahabari kuhusu wahalifu mbalimbali waliotiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
WATU 6
wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la kumshambulia
Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba
Msakuzi juziAkizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Selemani Kova amesema katika operesheni maalum iliyofanywa na jeshi la
polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao majina yako
yamehifadhiwa kwa sababu za usalama. Aidha Kamanda Kova aliongeeza kuwa
bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na uchunguzi
unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo.
VIJANA WAKUMBUSHWA KULINDA TASWIRA YA NCHI KIMATAIFA
-
Serikali imewataka vijana wanaopata fursa za ajira nje ya nchi kuwa
mabalozi wa Taifa kwa kuzingatia nidhamu, uadilifu na tamaduni katika nchi
wanazokwenda...
2 hours ago

No comments:
Post a Comment