Bila
shaka hili ni jambo ambalo mimi na wewe tulilitarajia. Baada ya maamuzi
ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya kuwavua madaraka ya kiuongozi waliyokuwa
nayo Mh.Zitto Kabwe na Dr.Kitila Mkumbo hapo jana, wawili hao wapo
tayari kukutana na waandishi wa habari na kuueleza umma maoni na msimamo
wao.
Katika
ujumbe mfupi ambao Mh.Zitto Kabwe ameuweka kwenye ukurasa wake wa
Facebook na taarifa hiyo hiyo kusambazwa kwa vyombo mbalimbali vya
habari, mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa kufanyika hapo kesho
saa tano [asubuhi] katika Hoteli Ya Serena jijini Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment