Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 16, 2013

AJAAT YATOA TUZO KWA WANAHABARI


AJAATMwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo (katikati)  akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi  wa Tume ya  Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) jana (leo) jijini Dar es salaam wa wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na AJAAT  kwa  mwaka 2013. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo.
CITIZEN
Mshindi wa Tatu wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI  kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la The Citizen Peter Muthamia(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu (300,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi  wa Tume ya  Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.HELEN Mshindi wa pili  wa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI  kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la TanzaniaDaima  Hellen Ngoromera (kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki tatu na nusu(350,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi  wa Tume ya  Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.JAMBOLEOMshindi wa  nne kwa Makala za mapambano dhidi ya UKIMWI  kwa upande wa magazeti ambaye pia ni Mwandishi wa Gazeti la Jamboleo Eben –Ezey Mende(kushoto) akipokea hundi ya shilingi laki mbili na nusu(250,000/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi  wa Tume ya  Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) baada ya kuwa miongoni mwa washindi.TACAIDSAMkurugenzi wa Habari na Uraghibishi  wa Tume ya  Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) Jumanne Isango(kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jana(leo)  jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa shindano la makala za UKIMWI lilioendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT)  kwa  mwaka 2013. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Mtendaji wa AJAAT  Simon Kivamo (katikati) na Meneja Mawasiliano wa AJAAT Perege Gumbo(kushoto)
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam

No comments:

Post a Comment