
Baadhi ya
vituo vikuu vya televisheni nchini Kenya vilisitisha matangazo yao
Jumatatu usiku baada ya mahakama kuu kutpilia mbali maombi yao ya kutaka
muda zaidi wa kubadilisha vyombo vya mfumo wa analog kuelekea mfumo wa
digital.
Mashirika
makuu ya Nation Media, Standard na Royal media service yaliwasilisha
maombi mbele ya mahakama kuu mwezi liyopita kutaka kupewa muda zaidi
kabla ya kubadilisha mfumo wa digitali ambao ulibidi kuanza Disemba 23,
2013 huko Kenya.
Kutokana
na hatua hiyo mamilioni ya watazamaji na mashabiki wa vituo vya NTV, KTN
citizen QTV na vituo vingine hawakuweza kuona matangazo yao na vipindi
wanavyopenda.
Baada ya
kushindwa mawakili wa vituo hivyo vitatu walisema hawana budi bali
kuheshimu sheria lakini wamesema wanafikisha malalamiko yao mbele ya
mahakama ya ruifaa Jumanne katika lengo la kubadili uwamuzi wa jaji
Majanja.
Mkurugenzi
mkuu wa Tume ya Mawasiliano Kenya CCK, Francis Wangusi anasema hatua
walochukua wamiliki wa vituo hivyo vya televisheni, kufunga matangazo
yao bila ya kushauriana na tume yake inakwenda kinyume na sheria . Na
watajaribu kujadiliana nao kufahamu kinachotendeka.
Jaji huyo alikataa pia
pendekezo la mashirika hayo ya televisheni kupewa muda wa siku 30 kuzima
matangazo yao ya analogue na kubadilisha katika digitali.
Kufuatana
na tume ya mawasiliano ya kenya CCK utaratibu ulibidi kuanza tarehe 13
disemba lakini mahakama ilichelewesha kwa siku 10 ili kusubiri uwamuzi
wa jaji hiyo Jumatatu.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)


No comments:
Post a Comment