FAMILIA ya Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi juzikati ilizua tafrani mtaani kufuatia
mzozo mkubwa wa nyumba kati ya mjukuu wa Mzee Mwinyi, Abdi Hassan
Mwinyi na
anayedai ni mmiliki wa kurithi, Edward Francis Bogwe.
Hii ndo nyumba yenyewe juzikati ilizua tafrani mtaani kufuatia
mzozo mkubwa wa nyumba kati ya mjukuu wa Mzee Mwinyi, Abdi Hassan Mwinyi na
anayedai ni mmiliki wa kurithi, Edward Francis Bogwe.
Tukio hilo lilijiri
mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwananyamala-Komakoma, Dar ambapo mtoto wa rais
mstaafu huyo aitwaye Abas Mwinyi aliongoza sekeseke mtaani.
Mtoto wa Mwinyi ( wa pili kutoka kushoto), Abas akiwa nyumbani
hapo.
Ishu ilikuwa hivi; miezi
kadhaa iliyopita, Edward alimfikisha Mahakama ya Ardhi chini ya Jaji Kombolwa,
Abdi akimtaka ahame kwenye nyumba hiyo ambayo ni mali ya familia, aliachiwa na
marehemu baba yake, Francis Bogwe.
Baada ya kusikiliza utetezi
wa pande zote mbili, mahakama ikaamuru Abdi ahame kwenye nyumba hiyo kwa vile
ni mali ya Francis.
Francis akiongozana na madalali alikwenda kumtoa Abdi na vitu vyake, ikiwemo familia na kupiga kufuli milango muhimu ya kuingilia ndani na kuondoka nyumba ikiwa tupu.
Francis akiongozana na madalali alikwenda kumtoa Abdi na vitu vyake, ikiwemo familia na kupiga kufuli milango muhimu ya kuingilia ndani na kuondoka nyumba ikiwa tupu.
Lakini siku mbili mbele,
Abas akiwa na ndugu zake wengine pamoja na askari kibao, sambamba na huyo Abdi
alifika akiwa na karatasi mkononi yenye maagizo kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha
Ardhi ikidai kuwa, Abdi aendelee kuishi ndani ya nyumba hiyo hadi keshi ya
msingi iliyofunguliwa na Abas ya kupinga kuhamishwa kwa Abdi itakaposikilizwa.
Kesi hiyo ilisikilizwa Desemba 2, mwaka huu kwenye mahakama hiyo jijini Dar.
Kesi hiyo ilisikilizwa Desemba 2, mwaka huu kwenye mahakama hiyo jijini Dar.
Baada ya kufika kwenye geti
la nyumba hiyo na kukuta watoto wa familia ya Bogwe, akiwemo dada wa Francis
aitwaye Josephine Bogwe, Abas alisema: “Shida yetu fungueni mlango tuingie
ndani hii ni nyumba yetu mambo mengine tutajuana mahakamani.” (huku akionesha
hati kutoka Mahakama ya Ardhi).
Baada ya kauli hiyo ndipo
tafrani ilipoibuka ambapo Josephine alitoa makaratasi yanayoonesha kuwa,
nyumba hiyo ni haki yao kama familia.
Josephine alimtaka Abas na
ndugu zake waoneshe vielelezo vyao vinavyoonesha kuwa nyumba hiyo ni yao.
“Hapa hadi kieleweke mnataka kutudhulumu haki yetu, haiwezekani mahakama itupatie haki nyinyi mnakuja na maaskari kuamuru nyumba ifunguliwe ili muingie ndani,” alisema Josephine.
“Hapa hadi kieleweke mnataka kutudhulumu haki yetu, haiwezekani mahakama itupatie haki nyinyi mnakuja na maaskari kuamuru nyumba ifunguliwe ili muingie ndani,” alisema Josephine.
Hata hivyo, katika kesi
iliyofunguliwa na Abas kwenye Mahakama Ardhi, Jaji Mziray alisema Abdi si
mmiliki halali wa nyumba hiyo kwa kuwa hana nyaraka zinazoonesha aliuziwa
nyumba hiyo na marehemu Francis.
Kwa upande wa Edward, Jaji Mziray alisema kwamba hakutakiwa kumuhamisha Abdi mara ya kwanza bila kupata hati ya hukumu akatakiwa kushughulikia hati hiyo kwanza.
Kwa upande wa Edward, Jaji Mziray alisema kwamba hakutakiwa kumuhamisha Abdi mara ya kwanza bila kupata hati ya hukumu akatakiwa kushughulikia hati hiyo kwanza.
Chanzo: GPL
No comments:
Post a Comment