Kwenye kundi hilo la A, Brazil anaonekana kama
mtemi baada ya kutwaa ubingwa huo mara tano, wakati wapinzani wake
hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kuwa bingwa.
Mabingwa watetezi, Hispania nao wamepangwa kwenye
kundi linalohitaji nguvu ya ziada kupenya baada ya kupangiwa timu za
Uholanzi, Chile na Australia kwenye Kundi B.
Staa wa Barcelona, Lionel Messi na Argentina yake
amepangwa kwenye Kundi F sambamba na timu za Nigeria, Iran na
Bosnia-Herzegovina, wakati mpinzani wake kwenye Ballon d’Or, Cristiano
Ronaldo na kikosi chake cha Ureno, anakabiliwa na mtihani mbele ya
Ujerumani, Ghana na Marekani kwenye Kundi G.
Kwenye makundi mengine, Uruguay, iliyotinga nusu
fainali kwenye fainali zilizofanyika Afrika Kusini miaka minne
iliyopita, itamenyana na Italia, Costa Rica na England kwenye Kundi D.
Ivory Coast imepangwa na Colombia kwenye Kundi C,
sambamba na timu za Japan na Ugiriki, wakati Ubelgiji itacheza na
Algeria, Korea Kusini na Urusi Kundi H.
Uswisi, ambayo kitendo cha kuingizwa kwenye chungu cha kwanza kiliibua mjadala, wamepangwa na Ufaransa, Ecuador na Honduras.
Brazil itaanza kwa kucheza na Croatia katika
Uwanja wa Arena Corinthians Juni 12, 2014 wakati Cameroon itakuwa
uwanjani siku inayofuata dhidi ya Mexico katika Uwanja wa Arenas das
Dunas.
Juni 13 kutakuwa pia na mechi ya Hispania dhidi ya Uholanzi na Chile dhidi ya Australia.
Mechi za makundi zitamalizika Juni 26, kupisha hatua ya 16 bora.chanzo MWANASPOTI.
TUNAOMBA BOFYAHAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUAAA(USIPITWEEE)
TUNAOMBA BOFYAHAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUAAA(USIPITWEEE)
No comments:
Post a Comment