Mwenyekiti wa mtaa wa pangani kata ya Makorongoni mjini Iringa Salum
Kibaya akiutazama mwili wa mtoto Raymond Ben Mangungu (2) aliyeuwawa kwa kukabwa shingo na baba wa kambo wakati wa ugomvi wa kimapenzi kati ya mwanaume huyo na mama wa mtoto huyo usiku wa leo.
Askari polisi akitazama mwili wa mtoto huyo.
Hali ilivyokutwa ndani ya chumba hicho baada ya tukio.
Wananchi wa Makorongini wakimtazama mwanamke huyo wakati akihojiwa na kaka wa mtuhumiwa wa mauwaji hayo.
Mama wa mtoto Raymond katikati akimsimulia shemeji yake jinsi ambavyo
mpenzi wake alivyoua mtoto ,kushoto ni mama mzazi wa mwanamke huyo.
Huyu ndie mzazi wa mtoto aliyeuwawa Bi Kudra Kahemela (23)
Wanawake wa mtaa wa Pangani Iringa wakiuhifadhi mwili wa mtoto Raymond leo.
KATIKA hali
isiyo ya kawaida mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Pangani kata ya
Makorongoni katika Manispaa ya Iringa Hamis Said maarufu kwa jina la
Mwarabu amemuua kinyama mtoto Raymond Ben Mangungu (2) kutoka na ugomvi
wa kimapenzi kati yake na mama wa mtoto huyo ambae kwake ni mpenzi wake .
Imedaiwa
kuwa mtuhumiwa huyo wa mauwaji ya mtoto huyo alikuwa amelewa pombe
kupita kiasi na si mara ya kwanza kulewa kiasi hicho na kutishia kufanya
mauwaji dhidi ya mtoto huyo wa kambo kwa kile alichokuwa akidai kuwa ni
fedhea kwake kuishi na mwanamke ambae ana watoto wawili ambao si damu
yake.
Wakizungumzia
juu ya tukio hilo mashuhuda wa tukio hilo kwa sharti la kutotaja majina
yao walisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa Mwarabu kumpiga mwanamke huyo
na familia yake kwa madai kuwa hataki kuwaona watoto hao wakiendelea
kuishi katika nyumba hiyo ambayo ameipanga yeye .
" Huyu
bwana Mwarabu alikuwa akifanya kazi ya kuuza korosho mitaani na akirudi
usiku amekuwa mkali kwa mwanamke huyo ambae alikuwa akidai kuwa bado
amekuwa na mahusiano na baba wa watoto hao wawili .....hata hivyo sisi
kama majirani tumekuwa tukishindwa kuwaamua kutokana na mwanaume kuwa na
tabia ya kulewa pombe kupita kiasi na hata tukio hili tulijua ni
kawaida yao "
Mtoto
Tinito Mangungu (6) ambae ni kaka na marehemu alisema kuwa baba yao huyo
mdogo alifika usiku na kuwataka wote kuamka kitandani na kuwa hakuna
mtu atakayelala katika chumba hicho kama si damu yake.
"Baba
mdogo (Mwarabu) alirudi usiku akiwa amelewa na kusema hakuna mtu kulala
kitandani na kuanza kumpiga mama kwa meza na viti huku sisi tukilia
kumtaka asimpige mama yetu....baada ya hapo alimchukua mdogo wangu na
kuanza kumkaba shingo na kumwacha kitandani akiwa amelama bila kuamka
hadi sasa mama anasema amekufa"
Akielezea
juu ya mkasa huo uliosababisha mauwaji ya mtoto Raymond mama mzazi wa
mtoto huyo Bi Kudra Kahemela (23) alisema kuwa kwa upande wake baada ya
kutishiwa kuuwawa kwa kipigo alifanikiwa kukimbia katika chumba hicho na
kwenda kujificha nje na baada ya muda mwanaume huyo alianza kutapika na
pale alipoingia kutana kumsaidia ndipo alipopigwa na kuamua kukimbia
kwenda kulala nje ya nyumba hiyo kwa kujiegesha katika nguzo ya umeme
iliyopo nyumba ya pili karibu na nyumba ya shekhe wa mkoa Juma Alli
Tagalile
Alisema
kuwa asubuhi aliingia katika chumba hicho baada ya mwanaume huyo kutoka
kwenda katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Tulivu kuendelea kunywa
pombe na kumkuta mtoto huyo akiwa amelala bila kutikisika .
" Mimi
nilijua kama mtoto amelala tu ama amezimia ila baada ya kuwaita watu
wazima akiwemo mama yangu mzazi ndipo nilipobaini kuwa mtoto wangu Ray
amefariki dunia na ndipo nilipomfuata na kumweleza juu ya tukio hilo ila
bado aliendelea kunywa pombe na kudai kuwa mtoto huyo amezimia kwa
kelele za usiku ."
Alisema
baada ya hapo mwanaume huyo alikimbia hadi Ilala kwa wakwe zake na
kuomba msamaha na kusuluhishwa ugomvi wao ila wakati mtengo wa kukamatwa
ukiwekwa ndipo alipokimbia kusiko julikana.
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia mtoto huyo akiwa amekufa katika kitanda cha
wazazi wake huku chini ya chumba hicho thamani mbali mbali pamoja na
vyombo vikiwa vimevunjika kutokana na ugomvi huo .
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa huo wa Pangani kata ya Makorongini Bw Salum Kibaya
amethibitisha juu ya kifo cha mtoto huyo na kuwa baada ya tukio hilo
ambalo lilitokea usiku wa kuamkia leo jumamosi Desemba 14 mwaka huu
alilazimika kwenda kituo cha polisi cha stendi kuu ya mabasi yaendeyo
mikoani na kuwajulisha juu ya tukio hilo na kufika eneo la tukio .
Bw Kibaya
alithibitisha pia kuwa ugomvi kati ya wapenzi hao si wa kwanza kutokea
japo kwa maelezo ya mwanamke huyo alikuwa mbioni kuolewa na mwanaume
huyo na hivyo kuwa na wanaume wawili akiwemo mzazi mwenzake ambae kwa
sasa anaishi eneo la Don Bosco mjini hapa.
Mwili wa
mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa huku
jeshi la polisi likiwahoji mama wa mtoto huyo ,kama wa mtuhumiwa wa
mauwaji hayo ambae ni mkazi wa Mlandizi Kibaha Jijini Dar es Salaam na
mama mzazi wa mtoto aliyepoteza maisha.
CHANZO NI FRANCIS GODWIN BLOG


No comments:
Post a Comment