Watu
kadhaa wamehofiwa kufariki kufuatia mlipuko uliotokea ndani ya gari
moja dogo la abiria katika mtaa wa Pangani mjini Nairobi.
Duru zinaarifu kuwa karibu watu 4 huenda wamefriki katika shambulizi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki.
Mlipuko
huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa
wa Eastleigh ambao una idadi kubwa ya wasomali wanaoishi huko.
Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.
Polisi
walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu
waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.
BBC SWAHILI


No comments:
Post a Comment