Ukiwa na roho nyepesi na mtu unayeumizwa roho kirahisi na maisha mazuri ya watu wengine, Instagram sio mtandao unaokufaa. Hata
hivyo, usiamini kila picha unayoiona kwenye Instagram. Hii ni kwasababu
watu wengi wamekuwa wakiitumia kuishi maisha fake na kuigiza ambayo
hayana hata asilimi 10 ya uhalisia. Unaweza ukaingizwa mkenge na picha
zinazooneshwa watu wakiishi maisha ya kifahari kumbe maisha yao halisi niya kustaajabisha.
Ipo
mifano mingi ya watu wanaoweka nyumba ama magari ya kufahari na kusema
ni yao wakati sio kweli. Instagram haiwezi kuonesha maisha halisi ya
watu japo baadhi ya wale wanaoonesha maisha ya kifahari kwa picha zao
wanayaishi kweli.
Ni sehemu ya kuonesha chakula kitamu ulichoagiza kwenye hoteli za bei za juu na kuwaumiza roho wengi.
Mtandao
huo wa kijamii umejipatia sifa ya kuonekana kuwa mtandao wa kishua
kuliko mingine yeyote. Hii ni kwasababu application yake inapatikana
kwenye smartphones peke yake, tofauti na mingine kama Facebook ambayo
Irene Uwoya anaichukulia kama ‘daladala’. Instagram imechuja watu na
kwa Tanzania imeonekana kupendwa.
Hiyo ndio sehemu iliyotawaliwa na selfie – picha za kujipiga mwenyewe, kawaida ama kusimama kwenye kioo.
Ni sehemu ambayo wasichana waliojaaliwa neema za Mungu huko nyuma kama akina Agnes Masogange, huitumia kunadi asset zao.
Instagram ni sehemu ya kuonesha mijengo inayojengwa na wasanii na watu wengine waliojaaliwa kipato.
Ni
sehemu ya kwanza kuiweka picha ya gari lako lako jipya ulilolinunua ili
kuwaonesha watu kuwa wewe si size yao, wewe ni matawi mengine kabisa.
Watajuaje
kuwa biashara ama mchongo unaofanywa umefanikiwa kama usipoweka picha
za noti nyingi za dola kama Irene Uwoya anavyoumiza roho za kwanini:
“Haya
wenye kuniagiza ndooomda huuu….minimemaliza kila kitu…afu bado pesa
nyingi zabak….inabidi ziiiiiiiishe….niagizen bwanaaaaa…….kama nawaona
wenye roho za kwanin…sio mim ni MUNGU,” ameandika Irene kwenye picha ya
chini aliyoiweka Instagram.
Ama
Diamond alivyoandika kwenye picha yake: Rubber band for what…???? Money
is tied by Money #USD #Gold #Valuables #WCB for Life mama.”
Au Jux alivyoweka picha hii:
Instagram ndio sehemu ya kuwaonesha watu nguo, viatu ama vidani aghali unavyovaa.
Kwa
mifano hiyo, picha hizi za kuumiza roho wengi zimepewa jina ‘braggie’
ikiwa na maana ya picha inayowekwa kwenye mitandao ya kijamii kushow off
ama kuwatia wivu washkaji, na kwa mujibu wa utafiti, mmoja kati ya
watuamiji 10 hufanya hivyo mara kwa mara.
Picha kama watu wakiwa kwenye vyumba vya hoteli, bar ama kwenye nightclubs si ngeni kwenye macho yako kama upo Instagram.CHANZO PAMOJA PURETUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment