Nelson Mandela ameongoza orodha ya majina yaliyotafutwa zaidi kwenye mtandao wa Google mwaka 2013. Orodha hiyo ya Google Zeitgeist imetoka jana Jumanne.
“Si
jambo la kushangaza kuwa trending search namba moja 2013 ilikuwa ni
alama ya kimataifa ya nguvu na amani: Nelson Mandela,” Makamu Mkuu wa
Rais wa Google, Amit Singhal alisema.
Nafasi
ya pili imekamatwa na muigizaji wa filamu ya The Fast and The Furious,
Paul Walker, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari mwezi uliopita. Nafasi
ta tatu imekamatwa na iPhone 5s.
Muigizaji wa Glee, Cory Monteith, aliyefariki kwa drug overdose mwezi July amekamata nafasi ya nne.
Nafasi
ya tano imekamatwa na Harlem Shake, ya sita Boston Marathon, ya saba
Royal Baby (Uingereza), ya nane Samsung Galaxy S4, ya tisa PlayStation 4
na ya 10 North Korea.


No comments:
Post a Comment