Kituo
cha Polisi cha Oysterbay, pamoja na nyumba za Polisi wanaoishi katika
Kambi hiyo, vitabomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa maduka ya kisasa
mfano wa Mlimani City ujenzi unaotarajia kuanza mwakani.
Tayari
baadhi ya askari waliokuwa wakiishi katika Kambi hiyo wameshapewa
'Notis' ili kuhama katika nyumba zao na wengine kubomoa wenyewe majengo
waliyokuwa wamejengwa kwa mabati katikati ya kambi hiyo ambayo walikuwa
wakiishi, ambapo wengi wao waliokuwa wakiisha katika nyumba za mabati
wamekwishabomoa nyumba zao na kuhama, huku baadhi wakiwa wamesalia
wakisubiri awamu ya pili. Askari hao wameelekezwa kuhamia katika nyumba
mpya zinazojengwa eneo la Kunduchi.
Baadhi
ya askari wamelalamikia utaratibu huo wa kuhamishwa katika eneo hilo,
hali ya kuwa pamoja na kubomolewa nyumba zao na Kituo cha Polisi, lakini
imeelezwa kuwa kitajengwa Kituo kipya kikubwa katika eneo hilo ambacho
kitajengea upande wa pili barabara ya Ubalozi wa Marekani.
Kinachowafanya
baadhi ya askari kulalamikia utaratibu huo ni kutokana na kujengwa tena
kituo kikubwa katika eneo hilo, lakini nyumba za askari zikiondolewa na
kutotakiwa kuwepo tena, ambapo askari wote watapewa nyumba Kunduchi na
kila atakayekuwa zamu atalazimika kusafiri ili kufika kazini, jambo
ambalo limeonekana ni usumbufu na hasa pale itakapotokea dharula za
kikazi.
Kamera
ya Sufianimafoto, ilibahatika kukatiza katikati ya kambi hiyo na
kushuhudia nyumba nyingi zikiwa tayari askari wameshahama huku zile za
mabati zikiwa zimebolewa na askari wakiwa tayari wamehama huku wengine
wakiendelea na zoezi la ubomoaji na kuhamisha mizigo yao kwa awamu.
HABARI ZAIDI BOFYA http://www.sufianimafoto.com


No comments:
Post a Comment