Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, December 6, 2013

Kocha mpya Azam FC aondoka... arudi kwao


Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Joseph Omog.
Na Martha Mboma
KOCHA Mkuu mpya wa Azam FC, Joseph Omog, ameondoka nchini kuelekea kwao Cameroon mara baada ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, kocha huyo ameondoka kwenda kupumzika na atarejea baada ya wiki mbili kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
“Kocha ameondoka Jumatano (juzi) kuelekea nchini kwake kwa ajili ya mapumziko ya wiki mbili kisha atarejea tena hapa nchini ili kuanza kukinoa kikosi chetu.
“Baada ya kurejea, ataendelea na majukumu yake kama kawaida na kuweka mikakati na mipango madhubuti kwa ajili ya timu yake na hata kuweza kufahamu anajipanga vipi katika kuhakikisha anaifikisha timu mbali,” alisema mtoa taarifa wetu.


TUNAOMBA BOFYAHAPA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUA(USIPITWEEEEE)

No comments:

Post a Comment