Mwenyekiti
Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza
na waandishi wa Habri jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la
kulaani kwa kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania,
Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwazalilisha Wabunge wa upinzani akiwepo
Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Picha na
Venance Nestory
Dar
es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim
Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya
kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.
Profesa
Lipumba ambaye pia ni profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es
Salaam kuwa hali ya uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya
wananchi wengi kuwa magumu.
“Vijana
wa siku hizi wengi hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda
sivyo, ajabu ni kwamba wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi
wa kutetea kwa hoja zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,”
alisema.
Akizungumzia
maazimio yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa
la CUF kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema
hatua ya kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo
yanaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo
lingeweza kuzuilika kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.
Kuhusu
hali ya kisiasa nchini, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito
kwa vyombo vya Dola kuwa na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza
amri za wanasiasa zisizojali utawala wa sheria na haki za binadamu ili
vipunguze uhasama baina yao na raia.
“Serikali
pia isitumie Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia
masuala ya uvunjifu wa sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,
badala yake kazi hiyo ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu
za kisheria. Nao pia waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.
Alisema
CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi
hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu
isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment