Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mama Denise
Nkurunziza, Mke wa Rais wa Burundi (kushoto) pamoja na Mke wa Rais wa
Namibia Mama Penehupifo Pohamba muda mfupi kabla ya kuhudhuria sherehe
za kukabidhiwa tuzo za Uongozi Uliotukuka mwiswhoni mwa kikao cha siku
tatu cha wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia
kilichofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis The Palm iliyoko Dubai, Umoja
wa Falme za Kiarabu (URA) kuanzia tarehe 16 hadi 18, Desemba 2013.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokea tuzo ya Uongozi Uliotukuka kimataifa (Global
Inspirational Leadership Award 2013) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi Mheshimiwa Bibi Furo Giami,
mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki
ya Kati na Asia. Mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya
Kiuchumi na Uongozi (CELD), wakishirikiana na CEO Clubs Network na
African Leadership Magazine uliofanyika katika hoteli ya Atlantis The
Palm, huko Dubai , Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.) Tuzo hiyo imetolewa
tarehe 18.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo huko Dubai tarehe 18.12.2013.
Dr. Angela Moore, Balozi wa Hisani kutoka kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani akiwavisha nishani washindi wa Tuzo .
Wake
wa Marais kutoka Barani Afrika waliotunukiwa Tuzo na Kituo cha
Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi wakionyesha tuzo,nishani na hati
walizokabidhiwa kwa washiriki wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika,
Mashariki ya Kati na Asia na wageni wengine waliohudhuria sherehe ya
utoaji tuzo hizo huko Dubai tarehe 18.12.2013.
Baadhi
ya wajumbe na washiriki waliofuatana na msafara wa Mama Salma Kikwete
kwenye mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia
wakisherehekea na kumpongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,
wakiongozwa na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu
Mheshimiwa Mbarouk Mbarouk, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Uongozi
Uliotukuka kwenye ukumbi wa Atlantis The Palm hotel tarehe 18.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na watu aliofuatana nao kwenye
sherehe ya kupokea Tuzo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu wa wanawake
kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia uliomalizika tarehe 18.12.2013
huko Dubai, Umoja wa Falme Aza Kiarabu .
PICHA NA JOHN LUKUWI


No comments:
Post a Comment