Juma
Kaseja `Tanzania One` amekingiwa kifua na bosi wake ,Yussuf Manji baada
ya kufungwa mabao matatu jana kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe
Na Baraka Mpenja
MWENYEKITI
wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemkingia kifua mlinda mlango wao
mpya, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao matatu jana akiwa langoni
katika mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Sc
ambao Mnayama alishinda 3-1.
Mbao
ya Simba sc katika mechi ya jana yalifungwa na Amis Tambwe aliyepiga
mawili na kiungo Juma Awadh Issa, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel
Okwi.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, Manji amasema hawakumsajili Kaseja kwa
ajili ya kuifunga Simba SC, bali malengo yao ni kupata msaada wake
katika michuano mikubwa ya soka barani Afrika.
Baada
ya Yanga kufungwa jana, huku Kaseja akiwa langoni, katibu mkuu wa
baraza la wazee la klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali, iliulaumu uongozi
kwa kusema kuwa usajili wa kipa huyo ni makosa na hauna baraka zao.
Manji
amejibu mapigo na kueleza kuwa umri unazidi kumtupa mkono mzee
Akilimali kwani ameshindwa kukumbuka kuwa , huyo Ivo mwenyewe aliondoka
Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa
wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi dhidi ya Simba SC.
Pia
Manji alihoji wakati Simba ikisawazisha mabao yote matatu katika
mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara oktoba 20 dhidi ya Simba sc ,
Kaseja alikuwa langoni?.
Mwenyekiti
huyo alisema si jambo zuri kulaumiana pale yanapotokea makosa, bali ni
kuwa na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
“Tunaheshimu
uwezo wa Kaseja, thamani yake ni kubwa. Hakuna kipa yeyote nchini
aliyedaka mechi nyingi za kimataifa kama kipa huyu. Kamwe hatuwezi
kumshusha thamini yake na uwezo wake kwa kufungwa mabao matatu kwenye
mechi ya jana ambayo ilikuwa sawa na bonanza tu”. Alisema Manji.
Manji
alisema mechi ya jana walicheza kumfurahisha mdhamini wao, TBL, lakini
haikuwa na maana yoyote na matokeo ya kufungwa wala hayajawaingia
akilini.
Hata hivyo Manji amewapongeza Simba SC kwa kucheza soka safi, hivyo walistahili ushindi katika mchezo wa jana.
Kuelekea
ngwe ya lala salama ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa , Manji
alisema wataboresha timu pamoja na benchi la ufundi kwa tafsiri ya
kuwaondoa makocha wao Ernie Brandts na wasaidizi wake, Mzawa Fredy Felix
Minziro na Mkenya, Mkenya Razack Ssiwa
“Timu
itaenda tena Ulaya kuweka kambini kama walivyofanya waka jana. Naamini
tutajivua vizuri na kuwa makali zaidi kutetea ubingwa wetu na kufanya
vizuri michuano ya kimataifa”. Alisema Manji.
Ili
kuongeza makali, Yanga imesajili wachezaji watatu katika dirisha dogo
la usajili ambao ni mlinda mlango, Juma Kaseja, kiungo Hassan Dilunga na
mshambuliaji mahiri raia wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi.
Wachezaji hao walitumika jana, lakini hawakufua dafu mbele ya kikosi cha Simba Sc kilichoonekana kuwa bora zaidi Yanga.
No comments:
Post a Comment