Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema Operesheni Tokomeza Ujangili, ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na baadhi yao kuyakimbia makazi. Lembeli alisema watuhumiwa, walikamatwa, walipekuliwa na kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo.
"Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi, madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa Serikali, walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza," alisema Lembeli
Aliongeza; "Watuhumiwa waliokamatwa
walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi
na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao."
Lembeli alitoa mfano kuwa Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanawe wa kiume (11) akishuhudia huku akilazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake.
Alisema mwanamke mmoja wa Babati (jina tunalo) alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe zake, pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.
Aidha, baadhi ya wanawake walidai kubakwa na kulawitiwa huku wilayani Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)

No comments:
Post a Comment