skip to main |
skip to sidebar
Mfanyabiashara ajiua kwa risasi, mwingine achinjwa
Watu
wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea
mkoani Singida mwishoni mwa wiki likiwemo la mfanyabiashara kujipiga
risasi kichwani na mwingine huchinjwa shingo, kutolewa koromeo na ulimi.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Geofrey Kamwela alisema katika tukio la kwanza, mfanyabiashara Mashaka
Omari (30) alikutwa chumbani kwake Mtaa wa Ipembe akiwa amekufa baada ya
kujipiga risasi kichwani.
Alisema mfanyabiashara huyo alijiua kwa
kutumia bastola yake yenye namba TZ CA 895101 ambapo polisi walikuta
ganda moja la risasi iliyotumika lakini magazini ilikuwa na risasi 11,"
alisema Kamanda Kamwela.
Uchunguzi wa awali unaonesha marehemu
alikuwa na mgogoro kati yake na mtu mwingine ambaye hakutajwa kwa ajili
ya masuala ya kiusalama hivyo kusababisha ajiue.
"Marehemu aliacha
ujumbe huo wa maandishi kwenye gari lake namba T664 EES aina ya Toyota
RAV 4 ambalo alikuwa ameliegesha nje ya ofisi yake," alisema na kuongeza
kuwa, uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Katika tukio
lingine, mkazi wa Kijiji cha Sambaru, Wilaya ya Ikungi, Tatu Selemani
(42), alichinjwa shingo na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika
saa 1:30 asubuhi.
Kamanda Kamwela alieleza licha ya kuchinjwa shingo
pia marehemu alitolewa koromeo, ulimi, kuchunwa ngozi usoni na kutolewa
sikio la kushoto ambapo mwili wake ulikutwa umbali wa mita 80 kutoka
nyumbani kwake.
Alisema katika tukio hilo, mtu mmoja Amosi Shenan
maarufu kwa jina la 'Babu', mkazi wa kijiji hicho ambaye ni mume wa
marehemu, amekamatwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi bado unaendelea
Chanzo;Majira
No comments:
Post a Comment