Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda anayedaiwa kuwa meneja wa
zamani wa Jackie Cliff amesema hajapokea ujumbe wowote kutoka kwa
mwanadada huyo anayeshikiliwa kwa tuhuma za madawa ya kulevya huko
Macao, China alipokuwa akitokea nchini Thailand.
Martin Kadinda na JackieUjumbe ulidhaniwa umetumwa na Jackie kwenda kwa Martin baada ya kukamatwa
Martin ameiambia tovuti hii kuwa ujumbe uliosambaa katika mitandao, uliandikwa na Jackie mwaka 2010 ambapo alikuwa akimaanisha mambo yaliyokuwa ‘personal’ zaidi.
“Ujumbe uliosambaa ni wa Jackie kweli ila ni wasi kunyingi sana mwaka 2010. Kwahiyo watu walivyoona unafanana na tukio hili wakaona waambatanishe. Nakumbuka ujumbe huu aliuandika sio kwa tukio kama hili yalikuwa ni mambo ya personal,” amesema Martin.
Martin akiwa na Jack
Hata hivyo Martin amesema hawezi kuzungumzia suala la Jackie kukamatwa na dawa za kulevya kwakuwa yeye siyo msemaji.
Jackie Clifford FitzPatrick alikamatwa na madawa ya kulevya Dec 19 mwaka huu akitokea Thailand kwenda Macao alikokamatiwa huku wenzake wawili, Mtanzania na Mnaijeria wakikimbia
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment