Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 4, 2013

Misri yaandaa rasimu ya katiba mpya



C5BFBFE6-C3FB-4878-8678-8B8711F0DCE9_w640_r1_s_53e31.jpg
Jopo la wajumbe 50 limepitisha pendekezo la rasimu ya katiba mpya ya Misri itakayopigiwa kura na wananchi mapema mwakani.
Pendekezo hilo ni hatua ya awali katika juhudi za kurejesha utawala wa kidemokrasia baada ya kutimuliwa mwezi Julai kwa rais Mohamed Morsi. Pia itachukua nafasi ya katiba yenye utata iliyoidhinishwa na rais wa Kiislam Morsi.
Katiba mpya inataka uchaguzi wa rais na bunge kufanyika ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya wapiga kura kuipitisha.
Lakini itakuwa ni chaguo la rais wa mpito Adly Mansour kuamua ikiwa uchaguzi utafanyika kwanza.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUA(USIPITWEEEEE)

No comments:

Post a Comment