Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 5, 2013

Mizengo Pinda:: Mshahara wangu kama Waziri Mkuu hauzidi Shilingi milioni sita (6)




Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ameweka wazi mshahara wake anaolipwa kwa kuwatumikia wananchi wa Tanzania kama Waziri Mkuu. Mizengo pinda alidai kwamba analipwa kiasi cha
million sita ambao ni pamoja na posho ya mke wake.
Huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwani Waziri hajaona cha kuficha juu ya pesa anazopokea akiwa kama Prime Minister wa Tanzania akadai wanaodai analipwa zaidi ya hapo ni uzushi mkubwa kiasi kwamba yeye ni mkopaji tu katika mabenki na kuwa mshahara huo ni pamoja na mapato ya mkewe.

Akijibu maswali ya papo kwa papo, Mh. Waziri Mkuu amesema anapata take home ya shilingi milioni 6 za tz.. Anasema mshahara wake na wa Mh. Rais na makamu wake, hauna tofauti kubwa, haizidi tshng. Mil. 1.. Amemjibu Zito kwamba kwa kutaja uongo kiasi cha mshahara wake, Mungu atamhukumu.

Kaongezea kwamba yeye ni kati ya viongozi wanaokopa sana mabenki, pale maisha yanapomzidia. Na juzi juzi amechukua mkopo CRDB na NMB..



No comments:

Post a Comment