Jeshi
la polisi mkoani Arusha limemshikilia na kisha kumwachia “chapchap”
mtoto wa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro na
mfanyabiashara maarufu nchini,Oscar Themi kwa kosa la kumpiga risasi
ya kichwa mhudumu wa bar ya Empire iliyopo eneo la Shoprite jijini
Arusha.
Mtuhumiwa
huyo ,Dereck Themi alishikiliwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita
mara baada ya kutofautiana na mhudumu huyo wakati alipompatia bili ya
vinywaji aliyokuwa akitumia ndani ya bar hiyo kabla ya kumtandika
risasi.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mnamo
novemba 29 mwaka huu majira ya saa 7.30 usiku mtoto huyo wa kigogo
alimfyatulia risasi mhudumu huyo aliyetambulika kwa jina la Witness
Erasto wakati alipompatia bili ya vinywaji.
Mashuhuda
walidai kuwa kulitokea na hali ya tofauti kati yao ambapo Themi
alikubali kulipa bili hiyo ambapo alichukua fedha na kisha kumwekea
katika matiti yake na ghafla kuchomoa bastola yake na kisha kumtandika
eneo la kichwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mara baada ya tukio
hilo ndipo mtuhumiwa alijaribu kukimbia nje ya bar hiyo kuelekea usawa
wa eneo la maegesho la magari lakini kabla hajafika alifyatua risasi
nyingine zaidi ya tano hali iliyopelekea tafrani katika eneo la
Shoprite.
Hatahivyo,taarifa
hizo zimedai kuwa askari mmoja aliyekuwa akilinda benki ya Exim iliyopo
ndani ya eneo hilo la Shoprite alimvizia kimafia na kisha kumnyang”anya
bastola hiyo mtuhumiwa kabla ya kuwataarifu polisi waliofika eneo hilo
na kisha kumfikisha katika kituo kikuu cha polisi cha kati.
Mtuhumiwa
huyo alifikishwa katika kituo hicho na kisha kukabidhi bastoa hiyo
pamoja na maganda matano ya risasi ambapo baada ya muda aliwasili mdogo
wake aliyetambulika kwa jina la Bernad Themi aliyechukua mali zake na
fedha.
Akihojiwa
na gazeti hili majeruhi wa tukio hilo Erasto alisema kuwa hawezi
kuongea chochote kwa kuwa hali yake ni sio nzuri lakini alipotafutwa
mmiliki wa bar hiyo,Tumaini Ulomi alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa tayari wameshafungua mashtaka mbalimbali ikiwemo hasara
aliyoipata siku ya tukio.
Mmiliki
huyo alisema kuwa mara baada ya milio ya risasi kuanza kurindima ndani
ya bar yake wateja mbalimbali wakiwemo watalii walitokomea
kusikojulikana bila kulipa hali ambayo imemtia hasara kubwa.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema kwa kifupi kwamba bado wanafanya uchunguzi wa kina
kabla ya kulifikisha suala hilo mahakamani.
Credit :libeneke la kaskazini
Credit :libeneke la kaskazini


No comments:
Post a Comment