TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema
kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia
na wengine kupoteza sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba,
alisema uchaguzi huo utafanyika katika halmashauri 23 baada ya
kukamilisha taratibu zinazotakiwa.
Alizitaja kata hizo na halmashauri
zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na
Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).
Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti
(Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba),
Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na
Namikago (Nachingwea).
Kata nyingine ni Partimbo na Loolera
(Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga
(Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na
Nyasura (Bunda).
Alisema uteuzi wa wagombea udiwani
utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16
hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9.
No comments:
Post a Comment