Jeshi la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwaua
watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao majina yao hayajafahamika waliokuwa wakipanga kuvamia mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi Mkoani humo Evarist Mangala amesema tukio hilo
limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo katika kijiji Namba
Tisa, baada ya kutokea majibizano ya risasi baina ya matuhumiwa hao na
Askari wa Doria.
Mangala amesema watuhumiwa hao wanaokisiwa kuwa na umri kati ya miaka
25-30, wamekutwa wakipanga kufanya uhalifu katika mgodi huo, kabla ya
kuanza kurushiana risasi na Askari Polisi na hatimaye kuzidiwa nguvu na
kuuawa.
Amesema
awali jeshi la polisi lilipata taarifa kuhusu uhalifu unaotaka kufanyika
katika mgodi huo, na ndipo likafuatilia na kukuta watuhumiwa hao wakiwa
na mabomu matatu ya kurusha kwa mkono wakijiandaa kufanya uhalifu
katika eneo hilo.
Mangala ameongeza kuwa mbali na kukutwa na mabomu hayo ya kivita pia
wamekutwa na bunduki mbili za kivita aina ya SMG zenye namba za usajili
1972PX7482 na UC-17751998 pamoja na risasi 94 ndani ya magazine nne.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,PIA BOFYA HAYO MATANGAZO UNAYOYAONA KUJIFUNZA VITU VINGI(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment