Mtu aliyetuhumiwa kujaribu
kuiba pikipiki aina ya Bajaj maeneo ya Coco Beach Dar es Salaam akiwa tahabani
baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi maeneo ya
Msasani
jirani na Hospitali ya CCBRT hivi karibuni. Kwamujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo kijana huyo alikubwa na mkasa huo alipokuwa katika
harakati za kukimbia na inadaiwa alikuwa na hirizi inayomsaidia kuendelea
kupumua. Askari wa Kituo cha polisi cha Oysterbay walifanikiwa kumpeleka
Hospitali ya Mwananyamala na tutawajuza kama anaendelea na hali gani. Kwa
mujibu wa askari wa Kituo hicho wamethibitisha kumfikisha hospitalini na kwa
kuwa hakuna anayemtuhumu baada ya kupata kipigo kikali watafanya mchakato wa kumlinda
mpaka atoke hospitalini.
Wakazi wa Dar es Salaam
wakimwangalia kijana aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj baada
kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira. Japokuwa kuchukua sheria
mkononi ni uvunjaji wa sheria pia matukio ya mauaji ya jinsi hii yameendelea
kutokea bila huruma kwa jamii ya Watanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo
watu walikuwa na utamaduni wa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ama kwa
watendaji na haki kupatakana kwa watuhumiwa na wanaowatuhumu kuchukuliwa CHANZO TANZANIA NEWZ
No comments:
Post a Comment