Marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o enzi za uhai wake
Familia
ya Marehemu Oming'o ikiwa uwanjani wakati wa bonanza lililopewa jina la
OMING'O SOCCER BONANZA kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu Jacob Arid
kwa jina maarufu Oming'o lililofanyika kwenye kiwanja cha Segerea siku
ya jumapili December 22, 2013 . Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.
Msemaji
wa Timu ya Segerea Veterans Sports Club akizungumza jambo wakati wa
bonanza lililofanyika kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji mwenzao
aliyefariki akiichezea timu hiyo katika uwanja wa Segerea ulioko Tabata
jijini Dar es Salaam
Timu
kapteni wa Segerea Veterans Sports Club akizungumza na vyombo vya
habari wakati wa bonanza la OMING'O SOCCER BONANZA lililofanyika jana
kwenye kiwanja cha Segerea, Tabata jijini Dar es Salaam hapo jana.
Mechi
zikiendelea wakati wa bonanza la kumkumbuka mchezaji mwenzao
aliyefariki uwanjani akiichezea timu yake ya Segerea Veterans Sports
Club
Mchezaji wa timu ya Kigamboni akiwa ameumia wakati wa nusu fainali ya kwanza
Ilikuwa ni furaha baada ya timu ya Kigamboni kuingia Fainali
Ubishi katika mechi kama hizi huwa haukosekani lakina refa ndo ana maamuzi yote
Wachezaji
wa timu ya Segerea Veterans Sports Club wakishangilia baada ya kushida
ubingwa wa bonanza la OMING'O SOCCER BONANZA lililofanyika kwenye
kiwanja cha Segerea kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji mwenzao Oming'o
aliyefariki akiichezea timu hiyo ya Segerea Veterans Sports Club
Wachezaji
wa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kushinda fainali hiyo
walielekea meza kuu ilipokuwa picha ya mchezaji mwenzao marehemu Jacob
Arid kwa jina maarufu Oming'o na kumwombea mungu ampumzishe mahali pema.
Hapa ni furaha kwa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kuchukua ubingwa
Mmoja
wa mashabiki wa timu ya Segerea Veterans Sports Club akiwa amebeba
picha ya marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o baada ya
kumalizika kwa bonanza hilo
PICHA PAMOJA BLOG
No comments:
Post a Comment