Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 23, 2013

REAL MADRID WASHINDA 3KWA 2,RONALDO AVUNJA REKODI YA KUFUMANIA NYAVU REAL MADRID!!



Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
Cristiano Ronaldo ameifungia bao Real Madrid jana usiku na kuvunja rekodi ya mmoja wa washambuliaji waliopo katika orodha ya kufunga mabao mengi zaidi enzi zao wakisakata soka.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno amefunga mabao 164 katika michezo 151 na kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Mexico, Hugo Sanchez aliyefunga mabao 164 katika mechi 207.
Ronaldo ameingia katika orodha ya wafungaji wanne wa juu waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real, lakini amebakiwa na rekodi tatu kuzivunja, yaani ya Santillana mwenye magoli 186,  Alfredo Di Stefano magoli  216 na Raul aliyetia kambani magoli 228. 
Real Madrid waliwafunga Valencia mabao 3-2 jana, shukurani zimwendee Ronaldo kwa kichwa chake mahiri dakika ya 40  kufuatia mpira mzuri wa adhabu uliochongwa na Agel Di Maria alimbadili Gareth Bale katika mchezo huo.
Madrid walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa kinda wao mwenye miaka 20 Jese Rodriguez katika dakika ya 84.
Bao la kwanza lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 28 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Valencia.
 Mabao ya Valencia yalifungwa na Pablo Piatti dakika ya 34 na Jérémy Mathieu dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia jana: Guita, Pereira, Ruiz, Mathieu, Romeu, Feghouli, Bernat, Parejo (Banega, 84), Cartabia, Piatti (Guardado, 80), Jonas.
Kikosi cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Carvajal, 80), Ramos, Nacho, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria (Illarramendi, 87), Isco (Jese, 73), Ronaldo, Benzema.
Record: Cristaino Ronaldo's goal against Valencia saw him become the joint fourth top scorer in Real's historyRekodi: Bao la Cristiano Ronaldo jana usiku dhidi ya  Valencia limemfanya aungane na wafungaji wanne waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real Madrid
Jumping for joy: Ronaldo scored Madrid's second goal of the evening during the 3-2 win over ValenciaAkiruka kwa furaha: Ronaldo aliifungia bao la pili Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-2 jana usiku
Team effort: Ronaldo is congratulated by his team-mates after his goal gave Madrid a half-time leadJitihada ya timu: Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1
Ahead: Angel di Maria celebrates with left back Marcelo after opening the scoring for Real Madrid against ValenciaKifua mbele: Angel di Maria  na beki wa kushoto Marcelo  wakishangilia bao la Margentina huyo
Leveller: Valencia's Pablo Piatti (centre) celebrates with his team-mates after equalising at the MestallaAmesawazisha: Mchezaji wa Valencia,  Pablo Piatti (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kusawazisha bao
Game on: Valencia French defender Jeremy Mathieu clenches his fist after scoring on the hour markKipute kinaendelea: Beki wa Valencia, Mfaransa , Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 62
Winner: Striker Jese (left) celebrates with team-mate Luka Modric after clinching the victory for MadridMshindi: Mshambuliaji  Jese (kushoto) akishangilia  na mchezaji mwenzake Luka Modric baada ya kuifungia Madrid bao la ushindi
So close: Real Madrid defender Sergio Ramos puts his hands on his head after missing a good chance to scoreAaaah! nimekosaje?: Beki wa Real Madrid,  Sergio Ramos akishika kichwa chake baada ya kupoteza nafasi ya wazi  kufunga  bao
Challenge: Real Madrid midfielder Xabi Alonso gets the better of Valencia winger Pablo PiattiChangamoto: Kiungo wa Real Madrid ,  Xabi Alonso akimtoka winga wa Valencia  Pablo Piatti katika mchezo wa jana usiku

No comments:

Post a Comment