![]() |
| Marehemu Clement Mabina. |
Mwenyekiti wa
zamani wa chama cha mapinduzi(ccm) mkoa wa Mwanza Clement Mabina ambaye
pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza ameuawa na
wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.
Tukio la
kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa
katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana
na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo
lilitokea leo asubuhi katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa
wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya
saa mbili asubuhi.
ODC Mkapa
alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa
zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya
Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa eneo la
kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda kupanda
miti.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa
amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira
kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na
kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.
Taarifa
zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza
kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm alifika katika eneo hilo majira ya
asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama
ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina
yake na wananchi.
Baada ya
kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na
kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro
wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.
Baada ya
majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina
aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa
bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika
eneo hilo na kupoteza maisha.
Taarifa
hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio
hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha
mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha
kifo chake papo hapo.
Kabla ya
kurejea chama cha mapinduzi(ccm) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya
Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi
kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge
katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo
hilo Malaki Lupondije.



No comments:
Post a Comment