Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Japhet Lusingu akiongea na waandishi wa habari juu ya tukio la ajali ya
moto lilitokea katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
iliyotokea tarehe 03.12.2013 maeneo ya Ngarenaro jijini hapa. (Picha na Rashid
Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
WIZARA YA
MAMBO YA NDANI
JESHI LA
POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TAARIFA YA AJALI YA MOTO KATIKA OFISI ZA CHADEMA
NDUGU WANAHABARI, MNAMO TAREHE 03/12/2013 MUDA WA SAA 5:00
ASUBUHI, POLISI MKOANI HAPA TULIPOKEA TAARIFA JUU YA KUCHOMWA MOTO KWA JENGO
AMBALO LINA OFISI ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ZILIZOPO MTAA
WA NGARENARO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA.
MARA BAADA YA TAARIFA HIYO ASKARI WALIKWENDA KATIKA ENEO LA TUKIO
NA KUKUTA MOTO UMEZIMIKA. JENGO HILO AMBALO LINA UZIO MREFU WA MATOFALI NA GETI
MOJA LA MBELE LINA OFISI TATU ZA CHAMA HICHO AMBAZO NI OFISI ZA WILAYA, MKOA NA
KANDA YA KASKAZINI AMBAZO ZINATUMIA BAFU NA CHOO KIMOJA.
AIDHA UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA
ZIMAMOTO IMEGUNDUA MAMBO YAFUATAYO:-
KWANZA, OFISI HIZO ZINALINDWA NA WALINZI WA CHAMA HICHO “RED
BRIGADES” NA SIKU YA TUKIO MLINZI ALIYEKUWA ZAMU ALIKUWA KITUMBWIZI S/O BAHATI
(42) MKAZI WA OLASITI AMBAYE ALIINGIA KAZINI TAREHE 02/12/2013 MUDA WA SAA
12:00 JIONI NA KUTOKA TAREHE 03/12/2013 MUDA WA SAA 12:00 ASUBUHI. AIDHA OFISI
HIZO ZINA KATIBU MUHTASI MMOJA AITWAYE JENIFER D/O MWASHA (25) MKAZI WA
SOMBETINI AMBAYE UWA ANAINGIA KAZINI SAA 1:30 ASUBUHI KILA SIKU LAKINI SIKU YA
TUKIO ALIINGIA SAA 4:00 ASUBUHI.
PILI, UCHUNGUZI UMEENDELEA KUBAINI KUWA, HAKUNA MAHALI
PALIPOVUNJWA KUTOKA KWENYE UZIO WA OFISI HIZO KURUHUSU MTU/WATU KUINGIA NDANI.
TATU, MLANGO WA NYUMA WA OFISI HIZO KATIKA VERANDA KULIGUNDULIKA
TUNDU KATIKA DARI KUELEKEA BAFUNI TUNDU LENYE UPANA WA FUTI MOJA NA NUSU KWA
NUSU (11/2X1/2) AMBALO NI DOGO KIASI CHA KUTOWEZESHA MTU KUPENYA KUINGIA NDANI
YA OFISI HIZO.
NNE, NDANI YA BAFU KULIPATIKANA MAJIVU NA KWENYE SAKAFU NA JUU YA
SINKI YAKIWA MAKAVU BILA MAJI MAJI YOYOTE.
TANO, KUTA ZOTE ZA BAFU NA CHOO HAZIKUWA ZIMEUNGUA.
SITA, ENEO LILILOUNGUA KWENYE DARI NI 3/4 (ROBO TATU MITA) LENYE
UPANA WA MITA 1 KWA UREFU WA MITA 3.
SABA, ENEO AMBALO MOTO ULIONEKANA UMEWAKA, MBAO KATIKA DARI
ZILIONEKANA KUUNGUA UPANDE WA CHINI NA UPANDE WA JUU WA MBAO NA CEILING BOARD
HAZIJAUNGUA KUOMYESHA MOTO ULIANZIA CHINI.
NANE, KUMEPATIKANA KIPANDE CHA CHUMA KILICHOKUWA NA KARATASI
ZILIZOUNGUA PAMOJA NA TOCHI NDANI YA DARI ENEO AMBALO MOTO ULIKUWA UKIWAKA
LAKINI VITU HIVYO HAVIKUONYESHA DALILI ZA KUUNGUA AU KUSHIKA MOTO, NA
INAONYESHA VIMEWEKWA BAADA YA MOTO KUZIMWA.
TISA, KUNA UWEZEKANO MKUBWA MOTO HUO ULIZIMWA KWA KUTUMIA HEWA
CHAFU/CO2.
KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA KUWAHOJI
MLINZI WA OFISI HIZO KITUMBWIZI S/O BAHATI PAMOJA NA KATIBU MUHTASI JENIFER D/O
MWASHA, HUKU UPELELEZI ZAIDI JUU YA TUKIO HILO UKIENDELEA. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI (ACP) JAPHET LUSINGU
TAREHE 04/12/2013.
No comments:
Post a Comment