“PRESS RELEASE” TAREHE 20.12. 2013.
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA
-TUNDUMA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA.
MTOTO KALIBU S/O KIMWELU, MIAKA 6, MNYAMWANGA, MKAZI WA MTAA WA TAZARA
TUNDUMA ALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA KISU NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA. AIDHA WATU HAO WALIMNYONGA SISTA D/O NYILENDA, MIAKA 17,
MNYIHA, MFANYAKAZI WA NDANI [HOUSE GIRL] KWA KUTUMIA WAYA WA TELEVISHENI
ULIOKUWEPO SEBULENI. MBINU NI KUWAVAMIA WAHANGA WAKIWA NDANI NYUMBANI
KISHA KUWAUA KINYAMA. MIILI YA MAREHEMU WOTE ILIKUTWA SEBULENI. WAKATI
WA TUKIO BABA WA MTOTO AITWAE ESTON S/O KIMWELU,MIAKA 55, MNYAMWANGA,
DIWANI WA KATA YA MKANGAMO – CCM, MKAZI WA TAZARA ALIKUWA SHAMBANI
KIJIJI CHA KIPAKA NA MAMA WA MTOTO AITWAE TUMAINI D/O YOHANA, MIAKA 29,
MNDALI, KATIBU MUHTASI HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIKUWA
KAZINI. KATIKA TUKIO HILO WATU HAO PIA WALIIBA MABEGI MAKUBWA MAWILI
YENYE NGUO MBALIMBALI YALIYOKUWA KATIKA CHUMBA WANACHOLALA WATOTO.
CHANZO KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI MGOGORO WA
MUDA MREFU WA KIFAMILIA KATI YA MKE MKUBWA NA MDOGO KUFUATIA FAMILIA
YA MKE MKUBWA KUDAI KUTELEKEZWA NA KUNYIMWA MALI/MASHAMBA. WATUHUMIWA
WATANO WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. GABRIEL S/O
KIMWELU, MIAKA 19, MNYAMWANGA, MKULIMA 2. ENOCK S/O SIMWELU, MIAKA 23,
MNYAMWANGA, MKULIMA 3. ALEX S/O SIMWELU, MIAKA 16, MNYAMWANGA,
MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI SHULE YA SEKONDARI MPAKANI WOTE NI WATOTO WA
MKE MKUBWA, WAKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA 4. MUSSA S/O NGOBA, MIAKA
19, MNYAMWANGA, MKULIMA MKAZI WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA NA 5. PATRICK
S/O MSIGWA, MIAKA 18, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA
WOTE NI MAJIRANI NA MARAFIKI WA WATOTO HAO. MIILI YA MAREHEMU
IMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA UCHUNGUZI. KAIMU KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA SUALA LA MALEZI BORA KWA WATOTO
NA VIJANA WAO ILI WAKUE KATIKA MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA MATUKIO YA
UHALIFU. AIDHA ANASISITIZA ILI KUWA NA TAIFA LENYE USTAWI MZURI WA
JAMII SUALA LA MALEZI BORA KWA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE. PIA ANATOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUUNA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO ENEO LA STERIO KATA YA
RUANDA, TARAFA YA SISIMBA BARABARA YA SOKOMATOLA/MAFIATI JIJI NA MKOA
WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI LILIMGONGA
MTEMBEA KWA MIGUU BOSCO S/O SANGANO, MIAKA 45, MMATENGO, DAKTARI
MWANAFUNZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO
HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI NA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTU
ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE.
Signed by:
[B.N MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYATUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment