Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 16, 2013

TANZANIA YAPAA KIMATAIFA KATIKA ANGA LA FILAMU,ZEST FILM PRODUCTION YAFANIKISHA FILAMU YA VAGABONDI KUINGIA TUZO ZA AFRICA



Filamu iitwayo "VAGABOND"imefanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye tuzo  za Filamu bora afrika baada ya kufikia viwango vya kimataifa.Huwezi kuamini kama filamu hii imetengenezwa nchini Tanzania kutokana na ubora wake na uhalisia.Zest Film Production ndio watengenezaji wa filamu hii nzuri na ya kuvutia ambayo imeweza kuonyesha kwamba vipaji vya watanzania vinazidi kukua kila siku.Mhusika mkuu katika Filaamu hiyo kali ni Hemedi Suleimani ama maarufu "PHD" ambaye ndani ya filamu hiyo ameonyesha kipaji cha hali ya juu na cha kuvutia.Mkurugenzi wa Zest Film Production Bwana Mussa Muziba amesema nia na malengo ya kampuni yao ni kusaidia kuinua soko la filamu za kitanzania na pia kuwawezesha wasanii wetu kutambulika kimataifa kama walivyofanya kwenye filamu hii,Pia ameongeza kwamba huu ni mwanzo tu na wameomba watanzania wasisite kushirikiana nao kwa maoni na ushauri ili kukuza soko la sanaa yetu.


No comments:

Post a Comment