Timu
ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeshika nafasi ya nne
michuano ya Kombe la Chalenji 2013 iliyofanyika nchini Kenya baada ya
kufungwa na timu ya Zambia kwa penalti 6-5. Dakika 90 za mchezo
zilimalizika kwa bao 1-1.
Bao la
Zambia lilifungwa na Ronald Kampamba katika dakika ya 51 kabla ya Kili
Stars kusawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta dakika ya 65 kipindi cha
pili.
Wachezaji
wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni,
Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi'. Waliokosa ni Haruna
Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.
No comments:
Post a Comment