Mpiga picha wa Clouds TV akiwajibika kuchukua tukio la ubovu wa stendi ya Njombe |
Abiria wakipita kwa shida katika stendi ya Njombe |
Mwanahabari wa Clouds TV na Radio Recho akitafuta eneo la kupita katika stendi hiyo ya Njombe |
Madereva
na abiria wanaotumia stendi ya Njombe mjini ambayo ni stendi kuu
ya mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia ubovu wa stendi hiyo na
kumwomba mbunge wa jimbo hilo Anne Simamba Makinda kushughulikia
tatizo hilo. Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com madereva hao na wananchi walisema kuwa ubovu wa stendi hiyo umekuwa ni kero kubwa kwao na kuiomba Halmashauri ya mji wa Njombe kulishughulikia suala hilo John Sanga ni mmoja kati ya madereva eneo hilo la stendi alisema kuwa wameshangazwa na hatua ya mbunge wao ambae ni spika wa Bunge kushindwa kuwajibika kwa kusimamia utengenezaji wa stendi hiyo. Kwa alisema wakati wa jua eneo hilo limekuwa likiongoza kwa kuwa na vumbi na wakati wa masika linaongoza kwa kuwa na tope sana . Hata hivyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya Njombe umekuwa ukitoa ahadi ya kutengeneza stendi bila kutekeleza kwa wakati na pale madereva wanapotaka kugoma wamekuwa wakitumia polisi kuwakamata waanzilishi wa migomo hiyo. Huku Sarah Ndelwa ambae ni mmoja kati ya abiria waliohojiwa akimtaka mbunge Makinda kusaidia kuondoa aibu hiyo ya ubovu wa stendi nyumbani kwake. TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE) |
No comments:
Post a Comment