Bwana mmoja aliefahamika kwa jina la Huan Chuncai mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa jimbo la Hunan anasumbuliwa na tatizo la nyama kukua kwa kasi katikakichwa chake hususan maeneo ya uso,ugonjwa
ambao
umetambulika kama neurofibromatosis ambao husababishwa na ukuwaji wa
cell ambalo ni moja ya matatizo ya kijetiksia. kwa mujibu wa the
dailymail kijana huyo amesumbuliwa na tatizo hilo toka angali mdogo
akiwa na umri wa miaka minne.Tayari amekwisha fanyiwa opesheni
mara
mbili kabla katika miaka tofauti tofauti (yaani mwaka 2007 na mwka
2008).Huan amepoteza meno yake yote akiwa na umri wa miaka 25 hali
inayompelekea apate shida kwenye kuongea pamoja na kula. Kijana huyo
ambae amekuwa akiitwa 'China's Elephant Man amekuwa akiishi kwa shida
sana,kwa mika mitano iliyopita nyama hizo zilikuwa na uzito wa 33lb
(15kg) na kumsababishia matatizo ya uti wa mgongo kupelekea maumivu
makali anayoyapata kutokana na kuongezeka kwa nyama hizo. Huan
amefanyiwa opesheni tena kuondoa nyama hizo kwa sasa zilizokuwa na uzito
wa 3.3lb (1.5kg). Opesheni yake huwa ni ya hatari sana kwani hupelekea
kuvuja kwa damu nyingi sana mwili mwake.
No comments:
Post a Comment