Samahani kwa muonekano wa picha hii ila ndio hali halisi Kiteto
Mauaji yakutisha Kiteto
· -- Wakulima wavamiwa, wachinjwa
· -Risasi za moto zatumika
· -Wachomewa nyumba zao
· -RC Manyara awasili kuwapa pole
Na Mohamed Hamad
WILAYA
ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya
kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi
Miongoni
mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa
(49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa
nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa
kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo
na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza
kunyinyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol kisha kuwasha moto
Akizungumza
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji
hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea
kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu
anachinjwa hadharani
“Nilichomewa
Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo
vyakula, lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema
najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema
chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao
kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya
kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga
uvamizi huo
Hata
hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa
kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa
madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana
Akielezea
hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya
Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi
kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja
Kwa
upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni
muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja
wahusika
Hata
hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti
huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya
kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa
kimasai
“Baada
ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka
twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha
wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya
kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu
saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji
Waliofariki
katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa
shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na
kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga
Waliolazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias
(21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma
Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu
Hata
hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika
kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka
utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze
kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi
wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani
maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe
huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja”alisema Mbwillo
No comments:
Post a Comment